Native Bible

Genesis 2:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi* ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.

Genesis 2:7 in English

Genesis 2:7 · Berean Standard Bible

Then the LORD God formed man from the dust of the ground and breathed the breath of life into his nostrils, and the man became a living being.*

Context

5hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi, 6lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi: 7Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi* ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai. 8Basi Bwana Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. 9Bwana Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.