Native Bible

Genesis 2:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi Bwana Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba.

Genesis 2:8 in English

Genesis 2:8 · Berean Standard Bible

And the LORD God planted a garden in Eden, in the east, where He placed the man He had formed.

Context

6lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi: 7Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi* ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai. 8Basi Bwana Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. 9Bwana Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya. 10Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.