Mwanzo 13:5
Genesis 13:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Basi Loti, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ngʼombe na mahema.
Genesis 13:5 in English
Genesis 13:5 · Berean Standard Bible
Now Lot, who was traveling with Abram, also had flocks and herds and tents.
Context
3Kutoka Negebu, akapita mahali hadi mahali, hadi akafika Betheli, mahali hapo ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati ya Betheli na Ai 4hapo ambapo alikuwa amejenga madhabahu ya kwanza. Huko Abramu akaliitia jina la Bwana. 5Basi Loti, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ngʼombe na mahema. 6Lakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao. 7Ukazuka ugomvi kati ya wachunga mifugo wa Abramu na wale wa Loti. Wakati huo, Wakanaani na Waperizi ndio waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.