Native Bible

Ezekiel 8:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Naye akaniambia, “Ingia ndani, ukaone maovu na machukizo wanayofanya humu.”

Ezekiel 8:9 in English

Ezekiel 8:9 · Berean Standard Bible

Then He said to me, “Go in and see the wicked abominations they are committing here.”

Context

7Kisha akanileta mpaka ingilio la ukumbi. Nikatazama, nami nikaona tundu ukutani. 8Akaniambia, “Mwanadamu, sasa toboa kwenye ukuta huu.” Ndipo nikatoboa ule ukuta, nikaona hapo pana mlango. 9Naye akaniambia, “Ingia ndani, ukaone maovu na machukizo wanayofanya humu.” 10Hivyo nikaingia ndani na kutazama, nikaona kuta zote zimechorwa kila aina ya vitu vitambaavyo na ya wanyama wachukizao wa kila aina na sanamu zote za nyumba ya Israeli. 11Mbele yao walisimama wazee sabini wa nyumba ya Israeli, naye Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama miongoni mwao. Kila mmoja alikuwa na chetezo mkononi na moshi wa harufu nzuri ya uvumba ulikuwa unapanda juu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.