Ezekieli 8:8
Ezekiel 8:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akaniambia, “Mwanadamu, sasa toboa kwenye ukuta huu.” Ndipo nikatoboa ule ukuta, nikaona hapo pana mlango.
Ezekiel 8:8 in English
Ezekiel 8:8 · Berean Standard Bible
“Son of man,” He told me, “dig through the wall.” So I dug through the wall and discovered a doorway.
Context
6Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, je, unaona yale wanayofanya, haya mambo ya machukizo kabisa nyumba ya Israeli wanayotenda hapa, ambayo yatanifanya niende mbali na mahali pangu patakatifu? Lakini utaona vitu ambavyo vinachukiza zaidi hata kuliko hivi.” 7Kisha akanileta mpaka ingilio la ukumbi. Nikatazama, nami nikaona tundu ukutani. 8Akaniambia, “Mwanadamu, sasa toboa kwenye ukuta huu.” Ndipo nikatoboa ule ukuta, nikaona hapo pana mlango. 9Naye akaniambia, “Ingia ndani, ukaone maovu na machukizo wanayofanya humu.” 10Hivyo nikaingia ndani na kutazama, nikaona kuta zote zimechorwa kila aina ya vitu vitambaavyo na ya wanyama wachukizao wa kila aina na sanamu zote za nyumba ya Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.