Native Bible

Ezekiel 8:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha akanileta mpaka ingilio la ukumbi. Nikatazama, nami nikaona tundu ukutani.

Ezekiel 8:7 in English

Ezekiel 8:7 · Berean Standard Bible

Then He brought me to the entrance to the court, and I looked and saw a hole in the wall.

Context

5Kisha akaniambia, “Mwanadamu, tazama kuelekea kaskazini.” Hivyo nikatazama na kwenye ingilio upande wa kaskazini wa lango la madhabahu, nikaona sanamu hii ya wivu. 6Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, je, unaona yale wanayofanya, haya mambo ya machukizo kabisa nyumba ya Israeli wanayotenda hapa, ambayo yatanifanya niende mbali na mahali pangu patakatifu? Lakini utaona vitu ambavyo vinachukiza zaidi hata kuliko hivi.” 7Kisha akanileta mpaka ingilio la ukumbi. Nikatazama, nami nikaona tundu ukutani. 8Akaniambia, “Mwanadamu, sasa toboa kwenye ukuta huu.” Ndipo nikatoboa ule ukuta, nikaona hapo pana mlango. 9Naye akaniambia, “Ingia ndani, ukaone maovu na machukizo wanayofanya humu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.