Ezekieli 43:16
Ezekiel 43:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pale pawashwapo moto pa madhabahu ni mraba, urefu wake ni dhiraa kumi na mbili* na upana wa dhiraa kumi na mbili.
Ezekiel 43:16 in English
Ezekiel 43:16 · Berean Standard Bible
The altar hearth shall be square at its four corners, twelve cubits long and twelve cubits wide.*
Context
14Kimo cha msingi kuanzia usawa wa ardhi mpaka kwenye mfereji sehemu ya chini kimo chake ni dhiraa mbili na upana wake ni dhiraa moja na kuanzia kwenye ukingo mdogo hadi kwenye ukingo mpana kimo chake ni dhiraa nne na upana wake ni dhiraa moja. 15Pale pawashwapo moto madhabahuni kimo chake kitakuwa dhiraa nne, na pembe nne zinazoelekeza juu kutoka pale pawashwapo moto. 16Pale pawashwapo moto pa madhabahu ni mraba, urefu wake ni dhiraa kumi na mbili* na upana wa dhiraa kumi na mbili. 17Pia sehemu ya juu ni mraba, urefu wake dhiraa kumi na nne na upana wa dhiraa kumi na nne, ikiwa na ukingo wa nusu dhiraa na mfereji kuizunguka madhabahu. Ngazi za kupandia madhabahuni zitaelekea upande wa mashariki.” 18Kisha akaniambia, “Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Haya ndiyo yatakayokuwa masharti ya kutoa dhabihu za kuteketezwa na kunyunyiza damu juu ya madhabahu itakapokuwa imejengwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.