Ezekieli 43:14
Ezekiel 43:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kimo cha msingi kuanzia usawa wa ardhi mpaka kwenye mfereji sehemu ya chini kimo chake ni dhiraa mbili na upana wake ni dhiraa moja na kuanzia kwenye ukingo mdogo hadi kwenye ukingo mpana kimo chake ni dhiraa nne na upana wake ni dhiraa moja.
Ezekiel 43:14 in English
Ezekiel 43:14 · Berean Standard Bible
The space from the gutter on the ground to the lower ledge shall be two cubits, and the ledge one cubit wide.* The space from the smaller ledge to the larger ledge shall be four cubits, and the ledge one cubit wide.*
Context
12“Hii ndiyo sheria ya Hekalu: Eneo lote linalozunguka Hekalu juu ya mlima litakuwa takatifu kuliko yote. Hii ndiyo sheria ya Hekalu. 13“Hivi ndivyo vipimo vya madhabahu kwa dhiraa ndefu, yaani, dhiraa moja na nyanda nne:* Tako lake liwe na kina cha hiyo dhiraa moja na upana wa hiyo dhiraa moja, ikiwa na ukingo wa shibiri moja* kuizunguka pembeni. Hiki kitakuwa ndicho kimo cha madhabahu: 14Kimo cha msingi kuanzia usawa wa ardhi mpaka kwenye mfereji sehemu ya chini kimo chake ni dhiraa mbili na upana wake ni dhiraa moja na kuanzia kwenye ukingo mdogo hadi kwenye ukingo mpana kimo chake ni dhiraa nne na upana wake ni dhiraa moja. 15Pale pawashwapo moto madhabahuni kimo chake kitakuwa dhiraa nne, na pembe nne zinazoelekeza juu kutoka pale pawashwapo moto. 16Pale pawashwapo moto pa madhabahu ni mraba, urefu wake ni dhiraa kumi na mbili* na upana wa dhiraa kumi na mbili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.