Ezekieli 40:10
Ezekiel 40:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndani ya lango la mashariki kulikuwepo vyumba vitatu vya kupumzikia kila upande, vyote vitatu vilikuwa na vipimo vilivyo sawa, nazo nyuso za kuta zilizotenganisha kila upande zilikuwa na vipimo vilivyo sawa.
Ezekiel 40:10 in English
Ezekiel 40:10 · Berean Standard Bible
There were three gate chambers on each side of the east gate, each with the same measurements, and the gateposts on either side also had the same measurements.
Context
8Kisha akapima baraza ya njia ya lango, 9ambayo ilikuwa na kina cha dhiraa nane* na miimo yake ilikuwa na unene wa dhiraa mbili.* Baraza ya lango ilielekea Hekalu. 10Ndani ya lango la mashariki kulikuwepo vyumba vitatu vya kupumzikia kila upande, vyote vitatu vilikuwa na vipimo vilivyo sawa, nazo nyuso za kuta zilizotenganisha kila upande zilikuwa na vipimo vilivyo sawa. 11Kisha akapima upana wa ingilio la lango, ilikuwa dhiraa kumi na urefu wake ulikuwa dhiraa kumi na tatu. 12Mbele ya kila chumba cha kupumzikia kulikuwepo ukuta uliokuwa na kimo cha dhiraa moja* kwenda juu, navyo hivyo vyumba vilikuwa dhiraa sita mraba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.