Native Bible

Ezekiel 40:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha akapima upana wa ingilio la lango, ilikuwa dhiraa kumi na urefu wake ulikuwa dhiraa kumi na tatu.

Ezekiel 40:11 in English

Ezekiel 40:11 · Berean Standard Bible

And he measured the width of the gateway entrance to be ten cubits,* and its length was thirteen cubits.*

Context

9ambayo ilikuwa na kina cha dhiraa nane* na miimo yake ilikuwa na unene wa dhiraa mbili.* Baraza ya lango ilielekea Hekalu. 10Ndani ya lango la mashariki kulikuwepo vyumba vitatu vya kupumzikia kila upande, vyote vitatu vilikuwa na vipimo vilivyo sawa, nazo nyuso za kuta zilizotenganisha kila upande zilikuwa na vipimo vilivyo sawa. 11Kisha akapima upana wa ingilio la lango, ilikuwa dhiraa kumi na urefu wake ulikuwa dhiraa kumi na tatu. 12Mbele ya kila chumba cha kupumzikia kulikuwepo ukuta uliokuwa na kimo cha dhiraa moja* kwenda juu, navyo hivyo vyumba vilikuwa dhiraa sita mraba. 13Kisha akapima njia ya lango kuanzia juu ya ukuta wa nyuma wa chumba kimoja cha kupumzikia hadi juu ya ukuta wa nyuma wa chumba upande wa pili; kukawa na nafasi ya dhiraa ishirini na tano kuanzia lango la ukuta mmoja hadi lango la ukuta uliokuwa upande mwingine.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.