Ezekieli 40:8
Ezekiel 40:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha akapima baraza ya njia ya lango,
Ezekiel 40:8 in English
Ezekiel 40:8 · Berean Standard Bible
Then he measured the portico of the gateway inside;*
Context
6Kisha akaenda kwenye lango linaloelekea mashariki. Akapanda ngazi zake akapima kizingiti cha lango, nacho kilikuwa na kina cha huo ufito. 7Vyumba vya kupumzikia vya walinzi vilikuwa na urefu wa huo ufito mmoja na upana wa huo ufito, kuta zilizogawa vyumba hivyo vya mapumziko zilikuwa na unene wa dhiraa tano.* Nacho kizingiti cha lango lililokuwa karibu na ukumbi unaoelekea hekaluni ulikuwa na kina cha huo ufito. 8Kisha akapima baraza ya njia ya lango, 9ambayo ilikuwa na kina cha dhiraa nane* na miimo yake ilikuwa na unene wa dhiraa mbili.* Baraza ya lango ilielekea Hekalu. 10Ndani ya lango la mashariki kulikuwepo vyumba vitatu vya kupumzikia kila upande, vyote vitatu vilikuwa na vipimo vilivyo sawa, nazo nyuso za kuta zilizotenganisha kila upande zilikuwa na vipimo vilivyo sawa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.