Ezekieli 37:5
Ezekiel 37:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa hii mifupa: Nitatia pumzi* ndani yenu, nanyi mtaishi.
Ezekiel 37:5 in English
Ezekiel 37:5 · Berean Standard Bible
This is what the Lord GOD says to these bones: I will cause breath * to enter you, and you will come to life.
Context
3Akaniuliza, “Mwanadamu, mifupa hii yaweza kuishi?”
Nikajibu, “Ee Bwana Mwenyezi, wewe peke yako wajua.” 4Ndipo akaniambia, “Itabirie mifupa hii na uiambie, ‘Enyi mifupa mikavu, sikieni neno la Bwana! 5Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa hii mifupa: Nitatia pumzi* ndani yenu, nanyi mtaishi. 6Nitawawekea mishipa, nami nitaifanya nyama ije juu yenu na kuwafunika kwa ngozi. Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtakuwa hai. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ” 7Basi nikatabiri kama nilivyoamriwa. Wakati nilipokuwa ninatabiri, kukawa na sauti, sauti ya kugongana, nayo mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.