Native Bible

Ezekiel 37:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo akaniambia, “Itabirie mifupa hii na uiambie, ‘Enyi mifupa mikavu, sikieni neno la Bwana!

Ezekiel 37:4 in English

Ezekiel 37:4 · Berean Standard Bible

And He said to me, “Prophesy concerning these bones and tell them, ‘Dry bones, hear the word of the LORD!

Context

2Akanipitisha pande zote kwenye hiyo mifupa, nami nikaona mifupa mingi sana ndani ya lile bonde, mifupa iliyokuwa imekauka sana. 3Akaniuliza, “Mwanadamu, mifupa hii yaweza kuishi?” Nikajibu, “Ee Bwana Mwenyezi, wewe peke yako wajua.” 4Ndipo akaniambia, “Itabirie mifupa hii na uiambie, ‘Enyi mifupa mikavu, sikieni neno la Bwana! 5Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa hii mifupa: Nitatia pumzi* ndani yenu, nanyi mtaishi. 6Nitawawekea mishipa, nami nitaifanya nyama ije juu yenu na kuwafunika kwa ngozi. Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtakuwa hai. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.