Ezekieli 37:3
Ezekiel 37:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akaniuliza, “Mwanadamu, mifupa hii yaweza kuishi?” Nikajibu, “Ee Bwana Mwenyezi, wewe peke yako wajua.”
Ezekiel 37:3 in English
Ezekiel 37:3 · Berean Standard Bible
Then He asked me, “Son of man, can these bones come to life?” “O Lord GOD,” I replied, “only You know.”
Context
1Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanitoa nje kwa Roho wa Bwana na kuniweka katikati ya bonde lililokuwa limejaa mifupa tele. 2Akanipitisha pande zote kwenye hiyo mifupa, nami nikaona mifupa mingi sana ndani ya lile bonde, mifupa iliyokuwa imekauka sana. 3Akaniuliza, “Mwanadamu, mifupa hii yaweza kuishi?”
Nikajibu, “Ee Bwana Mwenyezi, wewe peke yako wajua.” 4Ndipo akaniambia, “Itabirie mifupa hii na uiambie, ‘Enyi mifupa mikavu, sikieni neno la Bwana! 5Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa hii mifupa: Nitatia pumzi* ndani yenu, nanyi mtaishi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.