Ezekieli 32:15
Ezekiel 32:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa na kuiondolea nchi kila kitu kilichomo ndani yake, nitakapowapiga wote waishio humo, ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’
Ezekiel 32:15 in English
Ezekiel 32:15 · Berean Standard Bible
‘When I make the land of Egypt a desolation and empty it of all that filled it, when I strike down all who live there, then they will know that I am the LORD.’
Context
13Nitaangamiza mifugo yake yote
wanaojilisha kando ya maji mengi,
hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu
wala kwato za mnyama
hazitayachafua tena. 14Kisha nitafanya maji yake yatulie
na kufanya vijito vyake
vitiririke kama mafuta,
asema Bwana Mwenyezi. 15Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa
na kuiondolea nchi kila kitu
kilichomo ndani yake,
nitakapowapiga wote waishio humo,
ndipo watakapojua kuwa
Mimi ndimi Bwana.’ 16“Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asema Bwana Mwenyezi.” 17Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno la Bwana likanijia kusema:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.