Ezekieli 32:16
Ezekiel 32:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asema Bwana Mwenyezi.”
Ezekiel 32:16 in English
Ezekiel 32:16 · Berean Standard Bible
This is the lament they will chant for her; the daughters of the nations will chant it. Over Egypt and all her multitudes they will chant it, declares the Lord GOD.”
Context
14Kisha nitafanya maji yake yatulie
na kufanya vijito vyake
vitiririke kama mafuta,
asema Bwana Mwenyezi. 15Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa
na kuiondolea nchi kila kitu
kilichomo ndani yake,
nitakapowapiga wote waishio humo,
ndipo watakapojua kuwa
Mimi ndimi Bwana.’ 16“Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asema Bwana Mwenyezi.” 17Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno la Bwana likanijia kusema: 18“Mwanadamu, omboleza kwa ajili ya makundi ya wajeuri wa Misri na uwatupe kuzimu yeye na binti za mataifa yenye nguvu, waende huko pamoja nao washukao shimoni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.