Ezekieli 29:7
Ezekiel 29:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Walipokushika kwa mikono yao, ulivunjika na kuchana mabega yao; walipokuegemea, ulivunjika na migongo yao ikateguka.
Ezekiel 29:7 in English
Ezekiel 29:7 · Berean Standard Bible
When Israel took hold of you with their hands, you splintered, tearing all their shoulders; when they leaned on you, you broke, and their backs were wrenched.*
Context
5Nitakutupa jangwani,
wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako.
Utaanguka uwanjani,
nawe hutakusanywa au kuchukuliwa.
Nitakutoa uwe chakula
kwa wanyama wa nchi
na ndege wa angani. 6Ndipo wale wote waishio Misri watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.
“ ‘Umekuwa fimbo ya tete kwa nyumba ya Israeli. 7Walipokushika kwa mikono yao, ulivunjika na kuchana mabega yao; walipokuegemea, ulivunjika na migongo yao ikateguka. 8“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaleta upanga juu yako na kuua watu wako na wanyama wao. 9Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.
“ ‘Kwa sababu ulisema, “Mto Naili ni wangu; mimi niliufanya,”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.