Ezekieli 28:23
Ezekiel 28:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitapeleka tauni ndani yake na kufanya damu itiririke katika barabara zake. Waliochinjwa wataanguka ndani yake, kwa upanga dhidi yake kila upande. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.
Ezekiel 28:23 in English
Ezekiel 28:23 · Berean Standard Bible
I will send a plague against her and shed blood in her streets; the slain will fall within her, while the sword is against her on every side. Then they will know that I am the LORD.
Context
21“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake, 22nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni,
nami nitapata utukufu ndani yako.
Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana,
nitakapotekeleza hukumu zangu
na kuonyesha utakatifu wangu ndani yake. 23Nitapeleka tauni ndani yake
na kufanya damu itiririke katika barabara zake.
Waliochinjwa wataanguka ndani yake,
kwa upanga dhidi yake kila upande.
Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana. 24“ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana Mwenyezi. 25“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.