Ezekieli 28:20
Ezekiel 28:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Neno la Bwana likanijia kusema:
Ezekiel 28:20 in English
Ezekiel 28:20 · Berean Standard Bible
Then the word of the LORD came to me, saying,
Context
18Kwa dhambi zako nyingi na biashara yako ya dhuluma,
umenajisi mahali pako patakatifu.
Kwa hiyo nilifanya moto utoke ndani yako,
nao ukakuteketeza,
nami nikakufanya majivu juu ya nchi,
machoni pa wote waliokuwa wakitazama. 19Mataifa yote yaliyokujua
yanakustajabia;
umefikia mwisho wa kutisha
na hutakuwepo tena milele.’ ” 20Neno la Bwana likanijia kusema: 21“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake, 22nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni,
nami nitapata utukufu ndani yako.
Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana,
nitakapotekeleza hukumu zangu
na kuonyesha utakatifu wangu ndani yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.