Ezekieli 26:18
Ezekiel 26:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sasa nchi za pwani zinatetemeka katika siku ya anguko lako; visiwa vilivyomo baharini vinaogopa kwa kuporomoka kwako.’
Ezekiel 26:18 in English
Ezekiel 26:18 · Berean Standard Bible
Now the coastlands tremble on the day of your downfall; the islands in the sea are dismayed by your demise.”’
Context
16Ndipo wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuweka kando majoho yao na kuvua nguo zao zilizotariziwa. Wakiwa wamevikwa hofu kuu, wataketi chini ardhini, wakiwa wanatetemeka kila dakika na wakikustajabia. 17Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia:
“ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa,
ee mji uliokuwa na sifa,
wewe uliyekaliwa na mabaharia!
Ulikuwa na nguvu kwenye bahari,
wewe na watu wako;
wote walioishi huko,
uliwatia hofu kuu. 18Sasa nchi za pwani zinatetemeka
katika siku ya anguko lako;
visiwa vilivyomo baharini
vinaogopa kwa kuporomoka kwako.’ 19“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakapokufanya uwe mji wa ukiwa, kama miji isiyokaliwa tena na watu, nitakapoleta vilindi vya bahari juu yako na maji yake makuu yatakapokufunika, 20ndipo nitakapokushusha chini pamoja na wale washukao shimoni, kwa watu wa kale, nami nitakufanya uishi katika pande za chini za nchi kama katika magofu ya kale, pamoja na wale washukao shimoni, nawe hutarudi au kurejea kwenye makao yako katika nchi ya walio hai.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.