Native Bible

Ezekiel 24:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hivyo nikanena na watu asubuhi na jioni mke wangu akafa. Asubuhi yake nilifanya kama nilivyoamriwa.

Ezekiel 24:18 in English

Ezekiel 24:18 · Berean Standard Bible

So I spoke to the people in the morning, and in the evening my wife died. And the next morning I did as I had been commanded.

Context

16“Mwanadamu, kwa pigo moja nakaribia kukuondolea kile kilicho furaha ya macho yako. Lakini usiomboleze au kulia wala kudondosha machozi yoyote. 17Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya kawaida vya wakati wa matanga.” 18Hivyo nikanena na watu asubuhi na jioni mke wangu akafa. Asubuhi yake nilifanya kama nilivyoamriwa. 19Ndipo watu wakaniuliza, “Je, jambo hili unalofanya linamaanisha nini kwetu?” 20Kwa hiyo nikawaambia, “Neno la Bwana lilinijia kusema:

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.