Ezekieli 24:20
Ezekiel 24:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo nikawaambia, “Neno la Bwana lilinijia kusema:
Ezekiel 24:20 in English
Ezekiel 24:20 · Berean Standard Bible
So I answered them, “The word of the LORD came to me, saying:
Context
18Hivyo nikanena na watu asubuhi na jioni mke wangu akafa. Asubuhi yake nilifanya kama nilivyoamriwa. 19Ndipo watu wakaniuliza, “Je, jambo hili unalofanya linamaanisha nini kwetu?” 20Kwa hiyo nikawaambia, “Neno la Bwana lilinijia kusema: 21‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu na binti zenu mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga. 22Nanyi mtafanya kama nilivyofanya. Hamtafunika sehemu ya chini ya nyuso zenu wala hamtakula vyakula vya kawaida vya waombolezaji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.