Ezekieli 24:19
Ezekiel 24:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo watu wakaniuliza, “Je, jambo hili unalofanya linamaanisha nini kwetu?”
Ezekiel 24:19 in English
Ezekiel 24:19 · Berean Standard Bible
Then the people asked me, “Won’t you tell us what these things you are doing mean to us?”
Context
17Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya kawaida vya wakati wa matanga.” 18Hivyo nikanena na watu asubuhi na jioni mke wangu akafa. Asubuhi yake nilifanya kama nilivyoamriwa. 19Ndipo watu wakaniuliza, “Je, jambo hili unalofanya linamaanisha nini kwetu?” 20Kwa hiyo nikawaambia, “Neno la Bwana lilinijia kusema: 21‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu na binti zenu mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.