Ezekieli 23:15
Ezekiel 23:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wakiwa na mikanda viunoni mwao na vilemba vichwani mwao, wote walifanana na maafisa wa Babeli wapandao magari ya vita, wenyeji wa Ukaldayo.*
Ezekiel 23:15 in English
Ezekiel 23:15 · Berean Standard Bible
wearing belts on their waists and flowing turbans on their heads; all of them looked like officers of the Babylonians in Chaldea,* the land of their birth.
Context
13Nikaona kuwa yeye pia alijinajisi, wote wawili wakaelekea njia moja. 14“Lakini yeye akazidisha ukahaba wake. Akaona wanaume waliochorwa ukutani, picha za Wakaldayo* waliovalia nguo nyekundu, 15wakiwa na mikanda viunoni mwao na vilemba vichwani mwao, wote walifanana na maafisa wa Babeli wapandao magari ya vita, wenyeji wa Ukaldayo.* 16Mara tu alipowaona, aliwatamani, akatuma wajumbe kwao huko Ukaldayo. 17Ndipo hao Wababeli wakaja kwake kwenye kitanda cha mapenzi, nao katika tamaa zao wakamtia unajisi. Baada ya kutiwa unajisi, akawaacha kwa kuwachukia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.