Ezekieli 23:13
Ezekiel 23:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nikaona kuwa yeye pia alijinajisi, wote wawili wakaelekea njia moja.
Ezekiel 23:13 in English
Ezekiel 23:13 · Berean Standard Bible
And I saw that she too had defiled herself; both of them had taken the same path.
Context
11“Oholiba dada yake aliliona jambo hili, lakini kwa tamaa zake na ukahaba wake, akaharibu tabia zake kuliko Ohola dada yake. 12Yeye naye aliwatamani Waashuru, watawala na majemadari, mashujaa waliovalia sare, wapandao farasi, wanaume vijana wote waliovutia. 13Nikaona kuwa yeye pia alijinajisi, wote wawili wakaelekea njia moja. 14“Lakini yeye akazidisha ukahaba wake. Akaona wanaume waliochorwa ukutani, picha za Wakaldayo* waliovalia nguo nyekundu, 15wakiwa na mikanda viunoni mwao na vilemba vichwani mwao, wote walifanana na maafisa wa Babeli wapandao magari ya vita, wenyeji wa Ukaldayo.*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.