Ezekieli 23:16
Ezekiel 23:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mara tu alipowaona, aliwatamani, akatuma wajumbe kwao huko Ukaldayo.
Ezekiel 23:16 in English
Ezekiel 23:16 · Berean Standard Bible
At the sight of them, she lusted for them and sent messengers to them in Chaldea.
Context
14“Lakini yeye akazidisha ukahaba wake. Akaona wanaume waliochorwa ukutani, picha za Wakaldayo* waliovalia nguo nyekundu, 15wakiwa na mikanda viunoni mwao na vilemba vichwani mwao, wote walifanana na maafisa wa Babeli wapandao magari ya vita, wenyeji wa Ukaldayo.* 16Mara tu alipowaona, aliwatamani, akatuma wajumbe kwao huko Ukaldayo. 17Ndipo hao Wababeli wakaja kwake kwenye kitanda cha mapenzi, nao katika tamaa zao wakamtia unajisi. Baada ya kutiwa unajisi, akawaacha kwa kuwachukia. 18Alipofanya ukahaba wake waziwazi na kuonyesha hadharani uchi wake, nilimwacha kwa kumchukia, kama vile nilivyokuwa nimemwacha dada yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.