Ezekieli 18:3
Ezekiel 18:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli.
Ezekiel 18:3 in English
Ezekiel 18:3 · Berean Standard Bible
As surely as I live, declares the Lord GOD, you will no longer quote this proverb in Israel.
Context
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2“Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli:
“ ‘Baba wamekula zabibu zenye chachu,
nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’? 3“Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli. 4Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. 5“Mtu aweza kuwa ni mwenye haki
atendaye yaliyo haki na sawa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.