Ezekieli 18:2
Ezekiel 18:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli: “ ‘Baba wamekula zabibu zenye chachu, nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’?
Ezekiel 18:2 in English
Ezekiel 18:2 · Berean Standard Bible
“What do you people mean by quoting this proverb about the land of Israel: ‘The fathers have eaten sour grapes, and the teeth of the children are set on edge’?
Context
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2“Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli:
“ ‘Baba wamekula zabibu zenye chachu,
nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’? 3“Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli. 4Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.