Ezekieli 17:3
Ezekiel 17:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waambie hivi, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Tai mkubwa mwenye mabawa yenye nguvu, yaliyojaa manyoya marefu ya rangi mbalimbali, alikuja Lebanoni. Akatua kwenye kilele cha mwerezi,
Ezekiel 17:3 in English
Ezekiel 17:3 · Berean Standard Bible
and tell them that this is what the Lord GOD says: ‘A great eagle with great wings and long pinions,* full of feathers of many colors, came to Lebanon and took away the top of the cedar.
Context
1Neno la Bwana likanijia kusema: 2“Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli fumbo. 3Waambie hivi, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Tai mkubwa mwenye mabawa yenye nguvu, yaliyojaa manyoya marefu ya rangi mbalimbali, alikuja Lebanoni. Akatua kwenye kilele cha mwerezi, 4akakwanyua ncha yake na kuichukua mpaka nchi ya wafanyabiashara, akaipanda huko katika mji wa wachuuzi. 5“ ‘Akachukua baadhi ya mbegu za nchi yako na kuziweka katika udongo wenye rutuba. Akazipanda kama mti umeao kando ya maji mengi,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.