Ezekieli 1:26
Ezekiel 1:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi. Na juu ya kile kiti cha enzi kulikuwa na umbo mfano wa mwanadamu.
Ezekiel 1:26 in English
Ezekiel 1:26 · Berean Standard Bible
Above the expanse over their heads was the likeness of a throne with the appearance of sapphire, and on the throne high above was a figure like that of a man.
Context
24Viumbe wale waliposogea nilisikia sauti ya mabawa yao, kama ngurumo ya maji yaendayo kasi, kama sauti ya Mwenyezi,* kama makelele ya jeshi. Waliposimama kimya walishusha mabawa yao. 25Ndipo ikaja sauti toka juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao, waliposimama mabawa yao yakiwa yameshushwa. 26Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi. Na juu ya kile kiti cha enzi kulikuwa na umbo mfano wa mwanadamu. 27Nikaona kwamba kutokana na kile nilichoona kama kiuno chake kuelekea juu alionekana kama chuma inayowaka kana kwamba imejaa moto na kuanzia kiuno kwenda chini alionekana kama moto na mwanga mkali ulimzunguka. 28Kama vile kuonekana kwa upinde wa mvua mawinguni siku ya mvua, ndivyo ulivyokuwa ule mngʼao uliomzunguka.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa utukufu wa Bwana. Nilipouona, nikaanguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.