Native Bible

Ezekiel 1:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Viumbe wale waliposogea nilisikia sauti ya mabawa yao, kama ngurumo ya maji yaendayo kasi, kama sauti ya Mwenyezi,* kama makelele ya jeshi. Waliposimama kimya walishusha mabawa yao.

Ezekiel 1:24 in English

Ezekiel 1:24 · Berean Standard Bible

When the creatures moved, I heard the sound of their wings like the roar of many waters, like the voice of the Almighty,* like the tumult of an army. When they stood still, they lowered their wings.

Context

22Juu ya vichwa vya hao viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa eneo lililokuwa wazi, lililokuwa angavu kabisa na lenye kutisha. 23Chini ya hiyo nafasi mabawa yao yalitanda moja kuelekea jingine, kila mmoja alikuwa na mabawa mengine mawili yaliyofunika mwili wake. 24Viumbe wale waliposogea nilisikia sauti ya mabawa yao, kama ngurumo ya maji yaendayo kasi, kama sauti ya Mwenyezi,* kama makelele ya jeshi. Waliposimama kimya walishusha mabawa yao. 25Ndipo ikaja sauti toka juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao, waliposimama mabawa yao yakiwa yameshushwa. 26Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi. Na juu ya kile kiti cha enzi kulikuwa na umbo mfano wa mwanadamu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.