Native Bible

Exodus 6:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni.

Exodus 6:4 in English

Exodus 6:4 · Berean Standard Bible

I also established My covenant with them to give them the land of Canaan, the land where they lived as foreigners.

Context

2Pia Mungu akamwambia Mose, “Mimi ndimi Bwana. 3Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi,* ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao. 4Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni. 5Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu. 6“Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi Bwana, nami nitawatoa mtoke katika kongwa la Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.