Kutoka 6:3
Exodus 6:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi,* ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao.
Exodus 6:3 in English
Exodus 6:3 · Berean Standard Bible
I appeared to Abraham, to Isaac, and to Jacob as God Almighty,* but by My name the LORD I did not make Myself known to them.
Context
1Kisha Bwana akamwambia Mose, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.” 2Pia Mungu akamwambia Mose, “Mimi ndimi Bwana. 3Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi,* ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao. 4Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni. 5Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.