Native Bible

Exodus 40:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Fanyiza ua kuzunguka maskani na uweke pazia penye ingilio la ua.

Exodus 40:8 in English

Exodus 40:8 · Berean Standard Bible

Set up the surrounding courtyard and hang the curtain for the entrance to the courtyard.

Context

6“Weka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa mbele ya lango la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania; 7weka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, na uweke maji ndani yake. 8Fanyiza ua kuzunguka maskani na uweke pazia penye ingilio la ua. 9“Chukua mafuta ya upako, ipake Maskani ya Mungu pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake; iweke wakfu pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani mwake, nayo itakuwa takatifu. 10Kisha yapake mafuta hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka pamoja na vifaa vyake vyote; weka wakfu madhabahu nayo yatakuwa takatifu sana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.