Native Bible

Exodus 40:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Naye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao.

Exodus 40:31 in English

Exodus 40:31 · Berean Standard Bible

and from it Moses, Aaron, and his sons washed their hands and feet.

Context

29Mose akaweka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa karibu na ingilio la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka kama Bwana alivyomwagiza. 30Akaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia, 31Naye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao. 32Wakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu kama Bwana alivyomwagiza Mose. 33Kisha Mose akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Mose akaikamilisha kazi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.