Kutoka 35:9
Exodus 35:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
vito vya shohamu, na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani.
Exodus 35:9 in English
Exodus 35:9 · Berean Standard Bible
and onyx stones and gemstones to be mounted on the ephod and breastpiece.
Context
7ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo;* mbao za mshita; 8mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; 9vito vya shohamu, na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani. 10“Wote wenye ujuzi miongoni mwenu inawapasa kuja na kutengeneza kila kitu Bwana alichoamuru: 11Maskani pamoja na hema lake na kifuniko chake, vibanio, mihimili, mataruma, nguzo na vitako;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.