Kutoka 29:7
Exodus 29:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake.
Exodus 29:7 in English
Exodus 29:7 · Berean Standard Bible
Then take the anointing oil and anoint him by pouring it on his head.
Context
5Chukua yale mavazi na umvike Aroni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi. 6Weka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba. 7Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake. 8Walete wanawe na uwavike makoti, 9pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Aroni na wanawe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.