Kutoka 27:14
Exodus 27:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.
Exodus 27:14 in English
Exodus 27:14 · Berean Standard Bible
Make the curtains on one side fifteen cubits long,* with three posts and three bases,
Context
12“Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini,* nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi. 13Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini. 14Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 15Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano* kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 16“Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini* la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.