Kutoka 27:16
Exodus 27:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini* la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne.
Exodus 27:16 in English
Exodus 27:16 · Berean Standard Bible
The gate of the courtyard shall be twenty cubits long,* with a curtain embroidered with blue, purple, and scarlet yarn, and finely spun linen. It shall have four posts and four bases.
Context
14Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 15Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano* kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 16“Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini* la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne. 17Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba. 18Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.