Native Bible

Exodus 27:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba.

Exodus 27:17 in English

Exodus 27:17 · Berean Standard Bible

All the posts around the courtyard shall have silver bands, silver hooks, and bronze bases.

Context

15Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano* kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. 16“Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini* la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne. 17Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba. 18Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba. 19Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.