Kutoka 23:2
Exodus 23:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu,
Exodus 23:2 in English
Exodus 23:2 · Berean Standard Bible
You shall not follow the crowd in wrongdoing. When you testify in a lawsuit, do not pervert justice by siding with the crowd.
Context
1“Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine. 2“Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu, 3nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake. 4“Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.