Native Bible

Exodus 22:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba.

Exodus 22:25 in English

Exodus 22:25 · Berean Standard Bible

If you lend money to one of My people among you who is poor, you must not act as a creditor to him; you are not to charge him interest.

Context

23Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao. 24Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima. 25“Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba. 26Kama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama, 27kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.