Kutoka 21:24
Exodus 21:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,
Exodus 21:24 in English
Exodus 21:24 · Berean Standard Bible
eye for eye, tooth for tooth,* hand for hand, foot for foot,
Context
22“Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua. 23Lakini kukiwa na jeraha kubwa, ni lazima ulipe uhai kwa uhai, 24jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, 25kuchomwa moto kwa kuchomwa moto, jeraha kwa jeraha, mchubuko kwa mchubuko. 26“Ikiwa mtu atampiga mtumwa mwanaume au mwanamke kwenye jicho na kuliharibu, ni lazima amwache huru yule mtumwa kama fidia ya hilo jicho.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.