Kutoka 21:22
Exodus 21:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua.
Exodus 21:22 in English
Exodus 21:22 · Berean Standard Bible
If men who are fighting strike a pregnant woman and her child is born prematurely,* but there is no further injury, he shall surely be fined as the woman’s husband demands and as the court allows.
Context
20“Kama mtu akimpiga mtumwa wake wa kiume au wa kike kwa fimbo na mtumwa huyo akafa papo hapo, ni lazima aadhibiwe 21lakini ikiwa mtumwa ataamka baada ya siku moja au mbili, hataadhibiwa, kwa sababu yule mtumwa ni mali yake. 22“Ikiwa watu wawili wanapigana na wakamuumiza mwanamke mjamzito, naye akazaa kabla ya wakati lakini hakuna majeraha makubwa, mhalifu atatozwa mali kiasi cha madai ya mume wa yule mwanamke, na jinsi mahakama itakavyoamua. 23Lakini kukiwa na jeraha kubwa, ni lazima ulipe uhai kwa uhai, 24jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.