Native Bible

Exodus 17:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Huko nitasimama mbele yako karibu na mwamba wa Horebu. Uupige mwamba na maji yatatoka ndani yake kwa ajili ya watu kunywa.” Kwa hiyo Mose akafanya haya mbele ya wazee wa Israeli.

Exodus 17:6 in English

Exodus 17:6 · Berean Standard Bible

Behold, I will stand there before you by the rock at Horeb.* And when you strike the rock, water will come out of it for the people to drink.” So Moses did this in the sight of the elders of Israel.

Context

4Kisha Mose akamlilia Bwana, akasema, “Niwafanyie nini watu hawa? Sasa wanakaribia kunipiga kwa mawe.” 5Bwana akamjibu Mose, “Pita mbele ya watu. Wachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa Israeli, ichukue mkononi mwako ile fimbo uliyopiga nayo Mto Naili, nawe uende. 6Huko nitasimama mbele yako karibu na mwamba wa Horebu. Uupige mwamba na maji yatatoka ndani yake kwa ajili ya watu kunywa.” Kwa hiyo Mose akafanya haya mbele ya wazee wa Israeli. 7Naye akapaita mahali pale Masa,* na Meriba* kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu Bwana wakisema, “Je, Bwana yu pamoja nasi au la?” 8Waamaleki wakaja na kuwashambulia Waisraeli huko Refidimu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.