Native Bible

Exodus 17:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Naye akapaita mahali pale Masa,* na Meriba* kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu Bwana wakisema, “Je, Bwana yu pamoja nasi au la?”

Exodus 17:7 in English

Exodus 17:7 · Berean Standard Bible

He named the place Massah * and Meribah * because the Israelites quarreled, and because they tested the LORD, saying, “Is the LORD among us or not?”

Context

5Bwana akamjibu Mose, “Pita mbele ya watu. Wachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa Israeli, ichukue mkononi mwako ile fimbo uliyopiga nayo Mto Naili, nawe uende. 6Huko nitasimama mbele yako karibu na mwamba wa Horebu. Uupige mwamba na maji yatatoka ndani yake kwa ajili ya watu kunywa.” Kwa hiyo Mose akafanya haya mbele ya wazee wa Israeli. 7Naye akapaita mahali pale Masa,* na Meriba* kwa sababu Waisraeli waligombana na kumjaribu Bwana wakisema, “Je, Bwana yu pamoja nasi au la?” 8Waamaleki wakaja na kuwashambulia Waisraeli huko Refidimu. 9Mose akamwambia Yoshua, “Chagua baadhi ya watu wetu na uende kupigana na Waamaleki. Kesho nitasimama juu ya kilima nikiwa na fimbo ya Mungu mkononi mwangu.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.