Kutoka 17:4
Exodus 17:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kisha Mose akamlilia Bwana, akasema, “Niwafanyie nini watu hawa? Sasa wanakaribia kunipiga kwa mawe.”
Exodus 17:4 in English
Exodus 17:4 · Berean Standard Bible
Then Moses cried out to the LORD, “What should I do with these people? A little more and they will stone me!”
Context
2Kwa hiyo wakagombana na Mose wakisema, “Tupe maji ya kunywa.”
Mose akajibu, “Mbona mnagombana nami? Kwa nini mnamjaribu Bwana?” 3Lakini watu walikuwa na kiu huko, wakanungʼunika dhidi ya Mose, wakisema, “Kwa nini ulitutoa kule Misri, ukatuleta hapa utuue kwa kiu sisi, watoto wetu na mifugo yetu?” 4Kisha Mose akamlilia Bwana, akasema, “Niwafanyie nini watu hawa? Sasa wanakaribia kunipiga kwa mawe.” 5Bwana akamjibu Mose, “Pita mbele ya watu. Wachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa Israeli, ichukue mkononi mwako ile fimbo uliyopiga nayo Mto Naili, nawe uende. 6Huko nitasimama mbele yako karibu na mwamba wa Horebu. Uupige mwamba na maji yatatoka ndani yake kwa ajili ya watu kunywa.” Kwa hiyo Mose akafanya haya mbele ya wazee wa Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.