Native Bible

Exodus 16:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kisha Mose akawaambia, “Mtu yeyote asibakize chochote mpaka asubuhi.”

Exodus 16:19 in English

Exodus 16:19 · Berean Standard Bible

Then Moses said to them, “No one may keep any of it until morning.”

Context

17Waisraeli wakafanya kama walivyoambiwa, baadhi yao wakakusanya zaidi, wengine pungufu. 18Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji. 19Kisha Mose akawaambia, “Mtu yeyote asibakize chochote mpaka asubuhi.” 20Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Mose, wakahifadhi kiasi fulani mpaka asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Mose akawakasirikia. 21Kila asubuhi, kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji na jua lilipokuwa kali, iliyeyuka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.