Native Bible

Exodus 16:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji.

Exodus 16:18 in English

Exodus 16:18 · Berean Standard Bible

When they measured it by the omer, he who gathered much had no excess, and he who gathered little had no shortfall.* Each one gathered as much as he needed to eat.

Context

16Hivi ndivyo Bwana alivyoamuru: ‘Kila mmoja akusanye kiasi anachohitaji. Chukueni pishi* moja kwa kila mtu mliye naye katika hema yenu.’ ” 17Waisraeli wakafanya kama walivyoambiwa, baadhi yao wakakusanya zaidi, wengine pungufu. 18Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji. 19Kisha Mose akawaambia, “Mtu yeyote asibakize chochote mpaka asubuhi.” 20Hata hivyo, wengine hawakuzingatia aliyosema Mose, wakahifadhi kiasi fulani mpaka asubuhi, lakini kile alichohifadhi kikajaa mabuu na kuanza kunuka. Kwa hiyo Mose akawakasirikia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.