Kutoka 16:17
Exodus 16:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waisraeli wakafanya kama walivyoambiwa, baadhi yao wakakusanya zaidi, wengine pungufu.
Exodus 16:17 in English
Exodus 16:17 · Berean Standard Bible
So the Israelites did this. Some gathered more, and some less.
Context
15Waisraeli walipoona, wakaambiana, “Hiki ni nini?” Kwa kuwa hawakujua kilikuwa kitu gani.
Mose akawaambia, “Huu ndio mkate ambao Bwana amewapa mle. 16Hivi ndivyo Bwana alivyoamuru: ‘Kila mmoja akusanye kiasi anachohitaji. Chukueni pishi* moja kwa kila mtu mliye naye katika hema yenu.’ ” 17Waisraeli wakafanya kama walivyoambiwa, baadhi yao wakakusanya zaidi, wengine pungufu. 18Nao walipopima katika pishi, yule aliyekusanya zaidi hakuwa na ziada, wala aliyekusanya kidogo hakupungukiwa. Kila mmoja alikusanya kiasi alichohitaji. 19Kisha Mose akawaambia, “Mtu yeyote asibakize chochote mpaka asubuhi.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.